Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu illiyopo jijini Dar es Salaam imemruhusu mfanyabiashara James Rugemarila kuwasilisha hoja zake za kutaka aachiwe huru.
Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na wenzake wawili wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Maombi hayo ya Rugemarila ya kutaka kuwasilishwa kwa hoja zake za kuachiwa huru yamewasilishwa katika mahakama hiyo leo Februari 26 wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.