Hukumu ya Mbowe na wenzake kutolewa Machi Kumi

0
182

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es salaam, Machi Kumi mwaka huu inatarajia kutoa hukumu ya  kesi ya uchochezi inayowakabili  Viongozi nane wa Chama Cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt Vicent Mashinji.

Hatua hiyo imekuja baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kutoa siku tano kwa Mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za majumuisho juu ya shauri hilo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo  namba 112 ya mwaka 2018 ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika, Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Ester Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche.

Washitakiwa hao  wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwa ni pamoja na kufanya mkusanyiko na maandamano kinyume cha sheria  na kutoa maneno ya uchochezi.