Barabara kutoka Kimara hadi Golani yakarabatiwa

0
387

Wananchi wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kutunza miundombinu mbalimbali, ili miundombinu hiyo iweze kudumu kwa muda mrefu.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Golani manispaa ya Ubungo, – Dastan Patrick wakati wa ukarabati wa barabara ya Kimara hadi Golani iliyoharibiwa na mvua na kusababisha adha kubwa kwa Wakazi wa maeneo hayo.

Mwenyekiti huyo amepongeza utendaji kazi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na kuiomba Serikali kuwajengea barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Nao baadhi ya Wakazi wa mtaa huo wa Golani wameishukuru Serikali kwa kuwasaidia kukarabati barabara hiyo, huku wakisisitiza ombi lao la kutaka ijengwe kwa kiwango cha lami.