Hazard kukosa mchezo dhidi ya Manchester City

0
537

Nyota wa Real Madrid ya Hispania, Eden Hazard ataukosa mchezo wa wa Klabu Bingwa Ulaya (UCL) kati ya klabu yake dhidi ya Manchester City utakaopingwa Februari 26 katika dimba la Santiago Bernabeu kutokana na kuwa majeruhi.

Hazard aliumia kifundo cha mguu Jumamosi iliyopita wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza nchini Hispania (La Liga), ambapo Real Madrid ilikubali kipigo cha goli moja kwa bila kutoka kwa Levante.

Hazard mwenye umri wa miaka 29 aliumia katika kipindi cha pili cha mchezo huo na kutolewa uwanjani.

Mchezaji huyo amerejea dimbani siku za hivi karibuni baada ya kukaa nje kwa takribani miezi mitatu akiwa majeruhi.

Hazard, raia wa Ubelgiji ameichezea Real Madrid michezo 15 tangu ajiunge nayo akitokea Chelsea mapema mwaka 2019.