Tyson Fury bingwa WBC

0
348

Bondia Tyson Fury amemchapa kwa ‘Technical Knockout’ (TKO) mpinzani wake Deontay Wilder katika mzunguko wa saba wa pambano lililofanyika MGM Las Vegas, Marekani usiku wa kuamkia leo.

Kwa ushindi huo, Bondia Fury amechukua ubingwa dunia wa WBC, huku akimuachia majeraha Wilder kiasi cha kukimbizwa hospitali kutokana na kuumia sikio kiasi cha kushindwa kuongea na wanahabari baada ya mchezo.