Muziki wa Bongo wawapagawisha Wasanii Majuu

0
1420


Wasanii wa muziki nchini Marekani wameendelea kufurahia miziki ya Kibongo hasa ile miondoko ya Singeli ambayo ni maarufu zaidi maeneo ya uswahilini.


Katika video yake ya hivi karibuni, mtayarishaji wa muziki (Producer) kutoka nchini Marekani, – Swizz Beatz ameonekana akijirekodi na kufurahia wakati anasikiliza ngoma ya miondoko ya Singeli kutoka kwa Wanamuziki Meja Kunta na Lava Lava wa hapa nchini.


Mwanamama Alicia Keys naye pia hakuwa mbali, ameonekana kupagawa na kucheza wimbo wenye miondoko hiyo hiyo ya Singeli kutoka kwa Meja Kunta na Lava Lava.


Mtayarishaji huyo wa muziki Swizz Beatz hakuishia kwenye Singeli peke yake, pia ameposti video ya wimbo mpya wa Diamond Platnumz na mpenzi wake Tanasha Donna unaojulikana kama Gere.