Simba wazidi kujikita kileleni

0
383

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameendelea kupata ushindi katika michezo ya ligi kuu baada ya kuwachapa Biashara United ya Mara mabao 3-1 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Luis Miquissone kutoka Msumbiji, Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere na bao la tatu likifungwa na Mkenya Fransic Kahata.

Luis Miquissone akifurahia baada ya kufunga bao lake la kwanza

Simba inafikisha pointi 62, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 45 baada ya wote kucheza mechi 24 na kufanya tofauti ya point kuwa 17 baada ya Azam kupoteza mbele ya Namungo fc katika mchezo wa mapema