Timu ya Samatta yachezea kichapo Ligi Kuu England

0
411

Aston Villa imeendelea kuchechemea ligi kuu England baada ya kubamizwa mabao 2 kwa bila dhidi ya Southampton katika dimba la St. Mary’s

Kwa matokeo hayo Aston Villa wanaendelea kuning’inia juu ya mstari wa timu za kushuka daraja ikiwa na alama 25 baada ya kucheza michezo 27 wakiwa nafasi ya 17

Mechi nyengine zilizopigwa siku ya leo, Burnley imeshinda 3 bila dhidi ya AFC Bournemouth, Crystal Palace wakiibuka na ushindi wa bao moja bila dhidi ya Newcastle United huku Sheffield United wakitoka sare ya moja moja dhidi ya Brighton Hove Albion