CAF yamtema Drogba

0
475

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limemfuta kazi mmoja wa wateule wake Didier Drogba, kutoka katika nafasi ya kumshauri Rais wa shirikisho hilo, Ahmad Ahmad.

CAF imefikia uamuzi huo baada ya Drogba kushindwa kutimiza majukumu yake ya kumshauri rais huyo tangu alipoteuliwa mwezi Julai mwaka 2019.

Duru za kimichezo zinaarifu kuwa, nyota huyo mstaafu wa Ivory Coast pia ameshindwa kuhudhuria au kushiriki shughuli zozote za CAF ikiwemo michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2019.

Kwa sasa nafasi hiyo ya kumshauri Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika itabaki kwa mchezaji mstaafu wa Cameroon Samuel Eto’o.