Bashiru atua Mtwara

0
167

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally amewasili mkoani Mtwara kwa ziara ya siku tatu.

Katika uwanja wa ndege wa Mtwara, Dkt Bashiru amepokelewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho mkoani humo pamoja na mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM.

Akiwa mkoani Mtwara, pamoja na mambo mengine, kiongozi huyo atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya za Mtwara na Masasi, na kuzindua mashina ya wakereketwa wa CCM.