Serikali yatangaza ajira Elfu Moja za Madaktari

0
367

Rais John Magufuli ametangaza nafasi Elfu Moja mpya za ajira za madaktari nchini.

Rais Magufuli ametangaza nafasi hizo za ajira hii leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) na Rais Magufuli, mkutano unaofanyika pamoja na maadhimisho ya siku ya Madaktari Kitaifa kwa mwaka huu.

Rais Magufuli amesema kuwa, ametangaza ajira hizo mpya baada ya kubaini kuwa madaktari nchini hawatoshi.

Amesema kuwa Serikali itakua ikitangaza ajira zaidi za madaktari mwaka hadi mwaka ili kuhakikisha vituo vya afya, zahanati na hospitali zote zinazojengwa nchini zinakua na madaktari wa kutosha.