Zitto achukua fomu kutetea nafasi yake

0
264

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazaendo, Zitto Kabwe amechukua fomu ya kutetea nafasi yake ndani ya chama hicho.
 
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Kijitonyama jijini Dar es salaam, Zitto amesema kuwa amechukua fomu kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza chama hicho ili aweze kukamilisha malengo yake aliyojiwekea.
 
Jumla ya wanachama 58 wa ACT Wazalendo wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.

Uchaguzi wa chama hicho unatarajiwa kufanyika wakati wa mkutano mkuu wa chama utakaoanza Machi 14 hadi 16 mwaka huu.