Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amesema kuwa serikali itakamilisha ujenzi wa kiwanda cha Mwani kisiwani Pemba kama ilivyowaahidi wananchi.
Dkt Shein ameyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda uliofika Ikulu kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya mpango kazi kwa wizara hiyo katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2019.
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa Dkt Shein, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali amesema kuwa hadi kufikia Disemba mwaka 2019 wamefanikiwa kununua zaidi ya tani 1,600 karafuu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 20.3.