Maambukizi ya corona China yapungua na kuongezeka  

0
450

Kumekuwa na ongezeko jipya na maambukizi ya virusi vya corona nchini China, licha ya madaktari kutangaza kwa siku tatu mfululizo kuwa maambukizi yamekuwa yakipungua.

Madaktari nchini China walipata matumaini ya kukabiliana na virusi vya corona, baada ya mara ya kwanza maambukizi mapya kuonyesha dalili za kupungua, lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) likahadharisha kuwa kila nchi inatakiwa kuchukua tahadhari.

Shirika hilo lilisema kuwa kila nchi inatakiwa kuchukua tahadhari, kwani haifahamiki ni mwelekeo gani virusi hivyo vitakuja nao, baada ya kupunguza kasi yake kwa siku tatu mfululizo.

Wakati huo huo, abiria 99 waliokuwa kwenye meli moja ya kifahari ya Diamond Princes iliyokuwa imetia nanga katika bandari ya Yakohamaga nchini Japan, wamethibitika kuambukizwa virusi vya corona.

Abiria zaidi ya elfu tatu waliokuwa kwenye meli hiyo walilazimika kuwekewa karantini ya wiki mbili wakiwa ndani ya meli, ili madaktari wajiridhishe kama hawajaathiriwa na corona, kwa vile meli hiyo ilitokea China.

Tayari Marekani imepeleka ndege yake kuchukua raia wake waliokuwa katika meli hiyo ya kifahari na kuondoka nao, huku wagonjwa wakitengwa wakati wakisubiri matibabu, na abiria wengine walionusurika wakiwa katika uangalizi wa karibu wa madaktari.