Everton kuvunja mkataba na SportPesa

0
433

Klabu ya Everton ya nchini England imetangaza kufikia makubaliano na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kuhusu kuvunja mkataba wa udhamini mwishoni mwa msimu huu (2019/20).

Msemaji wa klabu hiyo amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa kufuatia mapitio ya kina ya mpango mkakati wake wa masuala ya kifedha, pia na kuzingatia malengo yao ya ukuaji.

Pande hizo mbili ziliingia mkataba wa miaka mitano mwaka 2017, ambapo uamuzi wa kuvunja mkataba huo umekuja ikiwa imesalia miaka miwili mkataba kufika mwisho.

Mkataba huo uliifanya Everton kuwa klabu ya kwanza kutoka England kuja Afrika Mashariki na kucheza na timu za ndani ambazo ni Gor Mahia, mwaka 2017 na Kariobangi Sharks FC, mwaka 2019, zote za Kenya, hatua iliyowasaidia kuongeza idadi ya mashabiki.

Pigo hilo kwa SportPesa limekuja siku chache baada ya Shirikisho la Soka la Ireland kuvunja mkataba nao.