Nyota wa filamu ya Queen of Katwe afariki dunia

0
1641

Muigizaji wa filamu maarufu ya Queen of Katwe, iliyotayarishwa chini Uganda na kampuni ya Disney kuhusu mchezo wa sataranji (chess) amefariki dunia akiwa na miaka 15.

Nikita Pearl Waligwa ambaye kwenye filamu hiyo aliigiza kwa jina la Gloria alikuwa akisumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye ubongo.

Katika filamu hiyo iliyohusu tukio la kweli alikuwa akielezea sheria za mchezo huo akiwa ni rafiki wa karibu wa nyota wa filamu, Phiona Mutesi ambaye alianza mchezo huo akiwa na miaka 9, na licha ya kuwa hakuwa na elimu aliweza kushinda mashindano ya kimataifa.

Nikita alibainika kuwa na uvimbe kwenye ubongo wake kwa mara ya kwanza mwaka 2016, ambapo mtayarishaji wa filamu hiyo, Mira Nair alichangisha fedha kwa ajili ya matibabu nchini India. Baada ya matibabu hayo aliambiwa kuwa yupo sawa, lakini mwaka 2018 alibainika kuwa na uvimbe mwingine.