Aston Villa yapoteza mchezo dakika za lala salama

0
363

Timu ya Aston Villa imeambulia patupu baada ya kukubali kipigo cha mabao 3 kwa mawili dhidi ya vijana wa Mourinho Tottenham Hotspur katika dimba lao la Villa Park

Mechi hiyo yakuvutia na kusisimua ilisubiri hadi 90 ili kumpata mshindi wa mchezo huo baada ya mchezaji Son kufunga bao la 3 na la ushindi kwa Tottenham katika dakika za nyongeza na kujizolea alama 3 muhimu zikiwafikisha Tottenham hadi nafasi ya 5 wakiwa na alama 40 nyuma ya chelsea wenye alama 41 katika nafasi ya nne

Aston Villa wanaendelea kushika nafasi ya 4 kutoka mwisho wakiwa na alama 25 wakisubiri mchezo wa West ham United kama wataendelea kubaki katika nafasi hiyo au watashuka kwenye mstari wa timu za kushuka daraja