Aliyedai kuwa na dawa ya kutibu corona aomba radhi

0
347

Mtumishi Moses Mollel maarufu kama Nabii namba Saba wa Kanisa la Huduma ya Neno na Maombi  lililopo wilayani Arumeru mkoani Arusha ,  ameomba radhi kwa Serikali na watu wote waliopata taharuki baada ya kutangaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa amepewa maono ya kutengeneza dawa inayotibu virusi vya Corona.

Baada ya kutoa tangazo hilo hivi karibuni, mtumishi huyo alikamatwa  na Jeshi la Polisi mkoani Arusha na kuhojiwa kwa muda wa saa Tisa kwa kosa la kutoa taarifa iliyozua taharuki miongoni mwa jamii.

Hata hivyo aliachiwa na yuko nje kwa dhamana, huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo.