Tanzania yasisitiza kutowaondoa wanafunzi waliopo Wuhan

0
401

Serikali imesisitiza kuwa, haina mpango wa kuwaondoa ama kuwasafirisha wanafunzi 420 waliopo katika jimbo la Hubei mji wa Wuhan nchini China, ambapo ndio kitovu cha maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuwa wako katika uangalizi maalum(karantini).


Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa, uamuzi huo Serikali unatokana  na taarifa za kitabibu zinazobainisha kutokea milipuko ya homa ya virusi hivyo katika mataifa ambayo awali yaliwaondoa Wananchi wao wakati wa mlipuko na kusababisha kusambaa kwa virusi hivyo na kuleta madhara zaidi kwa mataifa hayo.


Tanzania imesema inaheshimu masharti na mahitaji ya karantini iliyowekwa yanayozuia mtu yeyote kutoka ama kuingia katika mji huo kwa kusudi la kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo hadi hapo China itakapoondoa karantini hiyo. Serikali imewasihi wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi hao kuwa watulivu na kuepuka kutumika kisiasa kati.