Mgonjwa wa kwanza wa Corona barani Afrika apatikana Misri

0
517

Mgonjwa wa kwanza wa Corona amepatikana nchini Misri, na kuwa pia ni mgonjwa wa kwanza Barani Afrika.

Wizara ya afya ya Misri imeeleza kuwa, vipimo vya maabara vimethibitisha kuwepo kwa raia mmoja wa kigeni aliyetiliwa mashaka kukutwa na virusi hivyo vya Corona.

Tayari serikali ya Misri imekwishalijulisha Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu mgonjwa huyo.