Redio yaendelea kuwa na mchango katika jamii

0
367
Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Aisha Dachi

Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Aisha Dachi amesema kuwa, bado redio ina mchango mkubwa katika suala la upashanaji habari.

Dachi ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika mahojiano maalum na TBC ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani.

Amesema kuwa, kwa muda mrefu redio imekua ni njia nyepesi ya kufikisha ujumbe kwa watu mbalimbali kwa kuwa habari zake zimekua zikisambaa kwa haraka ndani ya jamii.

Siku ya Redio Duniani ilianzishwa mwaka 2012 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa ajili ya kusherehekea matangazo ya redio na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa miongoni mwa watangazaji wa redio.

Siku hiyo imekua ikisherehekewa Februari 13 ya kila mwaka.