Kwaheri Moi

0
618

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema atamuenzi  Rais wa awamu ya pili wa Taifa hilo Mzee Daniel Arap Moi kwa matendo yake mema ya upendo kwa wananchi wa Kenya, na watu wengine waliowahi kuwa karibu naye.
 
Kenyatta ametoa kauli hiyo kwenye Chuo Kikuu cha Kabarak nchini Kenya, muda mfupi kabla Mzee Moi hajazikwa nyumbani kwake huko Kabarak.
 
Moi amezikwa kwa heshima zote za Kiserikali, na mazishi yake kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Kenya, huku akipigiwa mizinga 19 kama ishara ya heshima ya uongozi kwa mwanasiasa huyo.
 
Rais wa awamu ya Tatu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa amemwakilisha Rais John Magufuli katika mazishi ya Mzee Moi, ambapo katika mahojiano na Mwandishi wa TBC jijini Nairobi amesema Marehemu atakumbukwa kwa misingi bora ya elimu aliyoweka katika Taifa hilo.
 
Mzee Moi amefariki dunia Jumanne wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 95.