Wanyamapori mbalimbali warejeshwa Ikulu Dar es salaam

0
264

Rais John Magufuli amerejesha wanyamapori katika bustani za Ikulu jijini Dar es salaam, hali iliyofanya mandhari ya eneo hilo kupendeza na kuvutia.

Wanyama waliopo katika bustani hizo ni pamoja na Pundamilia, Pofu, Swala, Digidigi, Tausi, Mbuni, Tumbili, Kanga na Batamaji.

Awali Wanyamapori hao walifugwa kwa idadi kubwa katika Ikulu hiyo ya Dar es salaam wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na baadaye walitoweka hadi mwaka 2017 walipoanza kurejeshwa na Rais Magufuli.

Hivi sasa katika maeneo ya Posta jijini Dar es salaam, kuna ongezeko kubwa la ndege aina ya Tausi ambao wanaonekana kuyapamba maeneo hayo.