Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mkewe Magreth, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais wa Pili wa Taifa hilo Mzee Daniel Arap Moi katika ukumbi wa Bunge jijini Nairobi.
Rais Kenyatta amewaongoza Raia wa Kenya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo, mwili ambao utalazwa katika Bunge hilo kwa muda wa siku Tatu kabla ya kuagwa Kitaifa Jumanne Februari 11.