Dkt Abbasi atoa maagizo kwa watumishi wa wizara ya habari

0
196

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezi, Dkt Hassan Abbasi amewaagiza watumishi walio chini ya wizara hiyo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa muda waliopangiwa.

Dkt Abbasi ameyasema hayo jijini Dodoma mara baada ya kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo baada ya kutoa na kusaini hati ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma.

Amesema muda ni kitu muhimu katika utekelezaji wa majukumu, hivyo ni muhimu kwa watumishi walio chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kulitambua hilo.

Dkt Abbasi amesema yeye kama mtendaji mkuu wa wizara asingependa kusikia mtumishi anachelewesha huduma kwa mteja kwa kisingizio cha mchakato na kwamba hatasaini wala hataingia mkataba na mtoa huduma yoyote kutoka sekta binafsi ambaye hajasaini hati ya uadilifu.