Baraza la Mawaziri Sudan lakutana kwa dharura

0
269

Serikali ya mpito ya Sudan imekuwa na kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri, baada ya Kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo kuanza kurejesha uhusiano na nchi hasimu ya Israel.

Taarifa ya jeshi la Sudan imesema kuwa, siku ya Jumatatu wiki hii ilikuwa ni ya kushangaza baada ya Kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo kuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel, – Benjamin Netanyahu.

Mazungumzo ya Viongozi hao wawili yalikuwa na lengo la kuimarisha ulinzi baina ya mataifa yao, hali iliyofanya awali Marekani kuitoa Sudan katika orodha ya mataifa ya kigaidi.

Kiongozi wa Sudan, -Abdul Fatah Al Burhani aliridhia anga la nchi hiyo kutumiwa na majeshi ya Israel.

Viongozi wa kiraia katika Serikali ya Sudan wameshutumu mazungumzo ya viongozi hao wawili na kusema kuwa hawakushirikishwa, hivyo hawayakubali.

Viongozi hao wawili walikutana mjini Entebe nchini Uganda.