CCM yapongezwa kwa kutimiza miaka 43

0
144

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais John Magufuli, amekipongeza chama hicho kwa kutimiza miaka 43 tangu kuzaliwa kwake.

Katika salamu zake kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Magufuli ametaka wakati wa kusherehekea siku hiyo muhimu kuendelezwa kwa misingi ya chama hicho na kusimamiwa kwa utekelezaji wa ilani ya CCM.

Pia ametaka Wananchama wote wa CCM kudumisha amani, upendo na mshikamano.

CCM ilizaliwa Februari Tano mwaka 1977 kutokana na kuungana kwa Chama cha TANU kilichokua kikitawala Tanzania Bara na ASP kilichokua kikitawala Zanziba kwa wakati huo.