Dkt Shein aipongeza Jumuiya ya Commonwealth

0
2287

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt  Ali Mohamed Shein ameipongeza Jumuiya ya Commonwealth kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kuwapongeza Maspika wa Mabunge ya Jumuiya hiyo kwa kufanya vikao vyao Zanzibar.

Dkt Shein ametoa pongezi hizo Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na viongozi wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Commonwealth kutoka nchi za Afrika  wakiongozwa na mwenyekiti wa viongozi hao ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,- Job Ndugai.

Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hao wamemweleza Dkt Shein kuwa Jumuiya ya Commonwealth inathamini na kutambua juhudi za Tanzania katika  kuiendeleza na kuiimarisha Jumuiya hiyo yenye historia kubwa.

Wakiwa Zanzibar, viongozi hao wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Commonwealth kutoka nchi za Afrika wamepata fursa ya kutembelea Baraza la Wawakilishi na kufanya mazungumzo na mwenyeji wao ambaye ni Spika wa Baraza hilo Zubeir Ali Maulid.

Pia wamefanya kikao cha kwanza cha Maspika wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Commonwealth kutoka nchi za Afrika.