Waliofariki Kilimanjaro waagwa leo

0
258

Shughuli ya kuaga miili ya watu ishirini waliofariki dunia kutokana na kukanyagana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, inafanyika mchana huu katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo katika Manispaa ya Moshi.

Habari kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa tayari miili hiyo imeondolewa kutoka katika Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro – Mawenzi kwenda kwenye viwanja hivyo vya Mashujaa.

Tukio la vifo vya watu hao lilitokea Jumamosi Februari Mosi mwaka huu wakati watu hao wakigombea kukanyaga mafuta yanayodaiwa kuwa na upako kwenye ibada iliyoendeshwa na Mtume na Nabii Boniface Mwamposa mjini Moshi.