Russia yashutumiwa kuanzisha vita ya kimtandao

0
2425

Shirika la kiintelijensia la Uingereza limeishutumu Russia kwa kuanzisha vita ya kimtandao dhidi ya mataifa ya Ulaya.

Shirika hilo limeishutumu Russia kwa madai ya kuanzisha vita hivyo ili kudidimiza demokrasia iliyo katika nchi za Ulaya.

Shirika hilo la kiintelijensia la Uingereza pia limeishutumu Russia  kwa kutumia baadhi ya vikundi vya watu na mashirika mengine kudukua taarifa muhimu katika nchi hizo za Ulaya.