Wapiganaji wa kikundi cha Houthi cha nchini Yemen wametangaza kuwa wamewaachia watoto wawili wa kiume wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Ali Abdallah Saleh waliokamatwa mara baada ya kifo cha baba yao.
Watoto hao wa Saleh walikamatwa mwezi Disemba mwaka 2017 mara baada ya wapiganaji hao kumuua baba yao.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa ndiye amekuwa akisimamia mazungumzo kati ya umoja huo na waasi hao wa kikundi cha Houthi yaliyosaidia kuachiwa kwa watoto hao.
Wapiganaji wa kikundi cha Houthi walimuua Saleh, baada ya kutoa wito wa kusimamisha mapigano nchini Yemen ili hatimaye amani irejee, jambo ambalo wapiganaji hao waliona kuwa ni usaliti.