Maalim Seif achukua fomu ya kugombea uongozi ACT Wazalendo

0
331

Katika kutimiza haki yake ya kidemokrasia Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amechukua fomu ya kugombea nafasi ya uwenyekiti ndani ya chama hicho leo Januari 30.

Maalim Seif ambaye amewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amechukua fomu hiyo kwenye ofisi ya chama hicho visiwani Zanzibar.

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi ya Taifa limeanza Januari 27 na litafikia tamati Februri 26 mwaka huu.