Makamu wa Rais ampa maelekezo waziri mpya wa muungano

0
225
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Muungano na Mazingira, Mussa Zungu aliyefika ofisini kwake kujitambulisha.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu ambapo amemtakia Waziri Zungu kila la heri katika utendaji wa majukumu yake na amemtaka afanye kazi kwa bidii.

Makamu wa Rais amekutana na waziri huyo alipofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kupokea maelekezo na utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri Zungu ameteuliwa kushika nafasi hiyo akichukua nafasi ya Waziri George Simbachawene ambaye amehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukua nafasi ya Kangi Lugola ambaye ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.