Hewa yenye uwezo wa kuhifadhi mbegu za uzazi yatengenezwa KCMC

0
257

HEWA ya naitrojeni yenye uwezo wa kuhifadhi mbegu za uzazi (za kiume na kike) imeanza kutengenezwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

Mwishoni mwa mwaka jana hospitali hiyo ilianzisha huduma ya uzazi kwa waliokosa mimba ambapo kliniki hufanyika mara moja kwa wiki.

Kliniki hiyo ilipoanza waliona wenza kati ya wanne hadi watano na sasa idadi ya wahitaji imeongezeka kufikia wenza 10 hadi 12 kwa siku.