Raia kutumika kupambana na makundi ya kigaidi Burkina Faso

0
354

Bunge nchini Burkina Faso limeidhinisha sheria  ya kuruhusu jeshi la nchi hiyo kutumia raia wanaojitolea  ndani ya jeshi ili kupambana na makundi ya kigaidi.

Waziri wa ulinzi nchini humo Cherif Sy amesema vijana hao wanaojitolea lazima wawe na umri kuanzia miaka 18 na watapatiwa mafunzo ya wiki mbili huku wakifanyiwa uchunguzi kabla ya kuanza kujiunga na jeshi nchini humo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia matukio ya mashambulizi ya mara kwa mara nchini humo pamoja na nchi jirani za Mali na Niger yaliyosababisha mauaji ya askari na raia.

Jumanne serikali ya nchi hiyo ilitangaza siku mbili za maombolezo kufuatia mashambulio katika vijiji viwili ambapo watu 36 walikufa.