Rais Magufuli aanika madudu Wizara mambo ya ndani

0
274

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameelezea kutoridhishwa na utendaji kazi wa viongozi wizara ya mambo ya ndani ya nchi baada ya kugundua makosa yaliyofanyika katika kuidhinisha mikataba iliyopo chini ya wizara hiyo

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa nyumba za maafisa na askari magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es salaam na kuwataka viongozi hao kuwajibika akiwemo Waziri Kangi Lugola

Aidha Rais Magufuli amesema katika kipindi cha miaka 4 kumekuwa na tume nyingi zilizoundwa ili kuichunguza wizara ya mambo ya ndani kutokana na miradi na mikataba ya hovyo

“Lugola nampenda sana ni mwanafunzi wangu nilimfundisha Sekondari , kwenye hili hapana , nilitegemea nisingemkuta hapa Kamishna Andengenye ni mchapakazi , nilitegemea hapa asiwepo,hatuwezi tukaendesha nchi kwa misingi ya ajabu”

Vile vile Rais Magufuli amelipongeza jeshi la kujenga taifa kwa kufanikisha ujenzi wa nyumba hizo kwa muda mfupi