Mawakili wa Rais Trump wataka kesi ifutwe

0
406

Mawakili wa Rais Donald Trump wa Marekani katika kesi inayomkabili mbele ya baraza la seneti na inayolenga kumuondoa madarakani, wamesisitiza kuwa rais huyo hajafanya kosa lolote.

Mawakili hao wamelitaka baraza la seneti kuifutilia mbali kesi hiyo kwa kuwa haina nguvu.

Wakati matayarisho ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo katika baraza la senate yakiendelea Kiongozi wa walio wengi katika baraza la Senate Mitch McConnell amewasilisha mpangilio wa namna ambavyo kesi hiyo itashughulikiwa, huku kura kuhusu mashahidi ikiahirishwa hadi wiki ijayo.

Makubaliano hayo yanawapa mawakili wa Trump nafasi ya kwanza kuwasilisha hoja zao na kuwaita mashahidi akiwemo mshauri wa zamani wa usalama wa taifa John Bolton aliyetakiwa kufika wiki ijayo.