Rais Magufuli afanya uteuzi

0
247

Rais Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti watano wa bodi za taasisi za Serikali baada yabodi za taasisi hizo kumaliza muda wake.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi
imeeleza kuwa wenyeviti hao wameongezewa muda baada ya vipindi vyao
vya awali kumalizika.

Rais Dkt Magufuli amemteua Agustino Mrema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole na Dkt. Harun Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania -TPC. Uteuzi wa Mrema na Dkt. Kondo umeanza leo.

Aidha Rais Magufuli amemteua Prof. Mayunga Nkunya kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi -NCC, Fidelis
Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa Mipango na
Matumizi ya Ardhi na Peter Maduki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo yaUfundiStadi -VETA.

Uteuziwa Prof. Nkunya, Mutakyamilwa na Maduki umeanza tarehe 17 Januari, 2020.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Noel Logwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa. Uteuzi wa Dkt. Logwa umeanza tarehe 17 Januari, 2020. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Logwa alikuwa
mhadhiri na mkuu wa idara ya akiolojia na mafunzo ya urithi ya Chuo
Kikuu cha DSM.

Dkt. LOGWA amechukua nafasi ya Prof. Audax Mabula ambaye amestaafu.