Uingereza yasaini makubaliano na Afrika ikielekea kujitoa EU

0
413

Uingereza imesaini makubaliano 11 ya kibiashara na baadhi ya nchi za Afrika, ikiwa ni wiki moja tu kabla taifa hilo halijajitoa ndani ya Umoja wa Ulaya (EU).

Nchi hiyo inatarajiwa kutangaza mkakati wake mpya wa maendeleo kwa Afrika leo Januari 20 unaotazamiwa kujikita zaidi kwenye maendeleo ya miundombinu na biashara.

Baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika wapo jijini London wanapohudhuria mkutano unaolenga kukuza uwekezaji wa Uingereza barani Afrika.

Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza imesema kwa sasa inaangazia zaidi kwenye teknolojia ya kidijitali, nishati mbadala na ujasiriamali wa wanawake.

Uhusiano baina ya Uingereza na Afrika unatarajiwa kubadilika mara baada ya nchi hiyo kujitoa ndani ya EU.