Dangote tajiri namba moja Afrika, Mo Dewji aendelea kutamba kwa vijana

0
488

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Forbes Bilionea Alliko Dangote (62) ametajwa kuwa tajiri namba moja Afrika akiwa na utajiri wa USD Billion 10.1, nafasi ya pili ikikamatwa na Nassef Sawiris (58) mwenye USD Billion 8 na nafasi ya tatu ni Mike Adenuga(66) USD Billion 7.7

Pia mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji (Mo) mwenye miaka 44 ametajwa kama bilionea namba 16 miongoni mwa mabilionea 20 wa Afrika kwa ripoti ya mwaka 2020 licha ya utajiri wake kupungua kwa Dola milioni 300 (Sh692.67 bilioni).

Utajiri wa Mo umetajwa kufikia Dola bilioni 1.6 (Sh3.69 trilioni) na anayeshikilia namba moja utajiri wake ni Dola bilioni 10.1 (Sh23.31trilioni) naye utajiri wake ukiwa umepungua kutoka bilioni 10.3 (Sh23.78 trilioni) mwaka jana.

Vilevile mfanyabiashara Mo Dewji ametajwa tena na ripoti mpya ya jarida la Forbes kuwa ni Mfanyabiashara tajiri mdogo kuliko wote Afrika kwa mwaka wa sita mfululizo akikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Billion 1.6 (Trilion 3.69 za Kitanzania)na kuendelea kubaki No.1 kwenye orodha ya Mabilionea wenye umri mdogo Afrika.