Mkuu wa Mkoa wa Geita aongoza wakazi wa wilaya ya Chato kujenga uzio wa shule ya Msingi Chato

0
209

Na Nazareth Ndekia, Chato Geita

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Chato wamelalamikia tabia ya wakazi wa maeneo ya jirani ya shule hiyo wengine hutumia vyoo vya shule na kupelekea vyoo hivyo kujaa mapema na wengine kuendesha bodaboda hukatiza katika shule hiyo wakati wanafunzi wakiendelea na masomo.

Wanafunzi wamesema hayo wakati wa ujenzi wa uzio wa shule hiyo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameongoza wananchi wa kijiji cha Mkuyuni kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi huo na wanafunzi hao wameishukuru serikali kwa kuona kero hiyo na kutafutia ufumbuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amezitaka halmashauri zote Mkoani humo kuhakikisha maeneo yenye miradi ya maendeleo yapimwe ili kuzuia wavamizi katika maeneo hayo kama shule,vituo vya afya.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chato Charles Kabeho amesema ujenzi wa uzio huo ukikamilika utaleta nidhamu kwa wanafunzi kutotoroka pamoja na wakazi kutoingilia mazingira ya shule.