Vikao vya kujadili hatma ya Rais Trump vyaanza

0
470

Jaji Mkuu wa mahakama ya juu nchini Marekani John Roberts pamoja na maseneta wameapishwa kuongoza vikao vinavyojadili hatma ya Rais Donald Trump ambapo wabunge wawili wa chama cha Democratic kutoka Bunge la wawakilishi wanaoongoza kesi hiyo dhidi ya Trump ni Adam Schiff wa Jimbo la California na Jerry Nadler wa New York.

Baada ya mashitaka hayo kusomwa vikao hivyo vimeahairishwa hadi Jumanne kwa kuwa bado kuna maamuzi ya usimamizi yanayopaswa kufanywa kuhusu jinsi vikao hivyo vitakavyoendelea.

Trump anadaiwa kuzuia USD 391 (TZS 902.8 bilioni) za msaada wa kijeshi ili kushinikiza Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, Joe Biden na tuhuma nyengine ni kuzuia bunge (congress) kufanya uchunguzi dhidi yake.

Hata hivyo Rais Trump amekanusha madai hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake ni udanganyifu unaofanywa na maadui zake.