Na Bertha Mwambela, Tanga
Jamii imetakiwa kutoingiza siasa katika suala zima la matibabu na badala yake imeombwa kuwekeza kwenye huduma za afya zilizoenea nchi nzima.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Tanga.
Konga amebainisha kuwa kwa sasa mfuko huo umeandaa kifurushi cha shilingi laki moja kwa waandishi wa habari ambacho kitamwezesha mwandishi wa habari kutibiwa kwa mwaka mzima.
Aidha, amesema wakati sasa umefika kwa watanzania kutumia vifurushi vya bima ya afya vilivyoboreshwa ili waweze kupata huduma stahiki na kwa wakati.