Mama amtelekeza mwanae hospitali kwa mujibu wa sheria

0
506

Mwanamke asiyefahamika amemtelekeza mwanae mwenye umri wa miezi miwili katika foleni ya kupata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Engela, Namibia.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na gazeti la The Namibian, mwaka 2019 serikali kupitia wizara ya jinsia ilihalalisha katika ibara ya 227 ya Sheria ya Ulinzi wa Mtoto kwamba watoto wanaweza kutelekezwa endapo tu wataachwa katika mazingira yaliyo sahihi..

Katika tukio hilo mwanamama huyo alimuomba mwanamke mwingine ambebe mwanae ili aende msalani, saa tatu baadae mama huyo hakuwa amerudi hali iliyompelekea mwanamke aliyeachiwa mtoto kutoa taarifa kwa manesi waliochukua hatua ya kuwajulisha polisi.

Naibu mkurugenzi wa huduma za watoto na ustawi katika Wizara ya Usawa wa Jinsia na Ustawi wa Watoto, Joyce Nakuta, amesema polisi hawana haja ya kumtafuta mwanamke huyo kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka, kwa kuwa amemwacha mtoto mahali salama.

Picha: Kutoka maktaba