Professor Jay afungua Studio muziki

0
1132

Mbunge wa Mikumi ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Hiphop Professor Jay amethibitisha kukamilika kwa studio ya muziki Mikumi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Professor Jay amepandisha video fupi inayoonesha studio mpya ya “Mwanalizombe Studios” ikiwa imekamilika.

Pia kwenye video hiyo anaonekana mtayarishaji Mr Ttouchez akijaribu baadhi ya vifaa.