Dkt Kipilimba na wenzake kuapishwa kuwa mabalozi

0
161

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Jumanne, Januari 14, 2020 anatarajia kuwaapisha mabalozi wateule wanne watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.

Wanaotarajiwa kuapishwa ni:

  1. Meja Jenerali (MST) Gaudence Milanzi, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Africa Kusini
  2. Dkt. Modestus Francis Kipilimba, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia
  3. Prof. Emmanuel David Mwaluko Mbennah, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe
  4. Dkt. Benson Alfred Bana, atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria