Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amewasili nchini Afrika Kusini kumuomba Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa kuingilia kati mgogoro wa ujenzi wa bwawa katika mto Nile unaozihusu nchi za Ethiopia, Misri na Sudan.
Waziri mkuu huyo, bwana Abiy Ahmed ameongea na Rais Cyril Ramaphosa juu ya ujenzi wa bwawa hilo ambalo nchi ya Ethiopia ilikubaliana na Misri kuwa ukamilike ndani ya miaka 12 lakini Misri imeona ni bora ujenzi huo kukamilika ndani ya miaka 21, jambo ambalo Ethiopia hawaafiki.
Ahmed amuomba Ramaphosa kuingilia kati kutokana na urafiki wa Afrika kusini, Ethiopia na Misri na pia kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anayetarajiwa kuanza rasmi muda wake mwezi wa Februari.
Mawaziri wa maji na nishati wa Misri Ethiopia na Sudan watakutana leo kujadili maendeleo yao mjini Washington.