Rais John Magufuli amesema Watalii wanakuja hapa nchini kwasababu kuna amani.
“Mtalii anakuja hapa nchini kwasababu anajua atakwenda kuogelea, kucheza, atakula chakula kizuri kwasababu kuna amani na inawezekana akatafuta mchumba mzuri au mshkaji akaondoka kwa amani yake” amesema Rais Magufuli
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Nyota Tano ya Verde Azam Luxury and SPA iliyopo eneo la Mtoni kisiwani Unguja