DC Tano Mwera ahamasisha zoezi la usajili wa NIDA Lamadi

0
191

MKUU wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera ametoa wito kwa wananchi wote wa Mji wa Lamadi na maeneo ya jirani kujitokeza kupata namba ya utambulisho wa uraia.

Zoezi hilo litaendeshwa kwa siku tatu na maafisa wa NIDA ambao wamepiga kambi mjini humo kwa lengo la kuhamasisha uandikishaji wa namba za uraia zinazotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

“Nachukua nafasi hii kuwahamasisha wana Lamadi wote ambao wanataka namba ya utambulisho wa uraia wafike katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata kwa wingi na watapata huduma hiyo kwa siku tatu,” alisema Tano Mwera.

Aidha, amesema kuwa baada ya zoezi hilo la muda wa siku tatu kumalizika katika Mji wa Lamadi na maeneo jirani ikiwemo Mkula, wananchi wataifuata huduma hiyo Nyashimo.