Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Ally Possi amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt Ayub Rioba kukamilisha mchakato na taratibu zote za kuhamia Dodoma.
Dkt Possi ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TBC Jijini Dodoma na kuongeza kuwa viongozi na watendaji wa TBC kupitia baraza hilo wajadili njia mbadala na bora zaidi yakuongeza mapato kwa shirika hilo.
Katika ufunguzi huo Dkt Possi amempongeza Mkurugenzi Mkuu kwa kuongeza usikivu kwa redio za TBC na kuboresha muonekano wa TBC1 huku akitimiza wajibu mkubwa na matakwa ya kisheria kwa kuandaa na kufanya baraza la wafanyakazi Jijini Dodoma.